Waziri wa Usalama na Masuala ya Ndani ya Nchi Kipchumba Murkomen amewaonya maafisa wa serikali dhidi ya kufanikisha shughuli haramu za unyakuzi wa ardhi katika Kaunti ya Kilifi.
Akizungumza katika ofisi ya kamishna wa Kaunti ya Kilifi, Murkomen amesema maafisa wa Idara ya Ardhi, Maafisa wa Idara mbalimbali za Utawala, wale wa Idara ya mahakama na hata polisi wamekuwa wakishirikiana na mabwanyenye kunyakua ardhi za wakazi.
Murkomen amesema inasikitisha kuona kuwa tatizo la unyakuzi wa ardhi limekuwa chanzo cha utovu wa usalama hasa katika eneo hilo la Pwani akisema walio hatarini zaidi ni wakongwe ambao baadhi wamedhulumiwa na wanao na hata jamaa zao wanaowapokonya ardhi kisha kuziuza.
Murkomen amesema ‘’ We need to tighten the controls when it comes to land issues because transfer of land is a legal process that requires a lot of consent along the way. But because there is collision of the sellers and the buyers we have a problem here, we have a lot of problems here that are related to land; insecurity is also perpetuated by issues related to land’’
Kuhusu suala la Shakahola Murkomen amesema serikali itatenga fedha katika bajeti ili kufanikisha uchunguzi unaoendelea. Amesema fedha hizo zitatumika kugharamia uchunguzi wa DNA pia kujenga eneo maalum kwa ajili ya ukumbusho kwa waathiriwa (memorial site in honour of the victims)
Wakati uo huo, ametoa wito kwa Idara ya Mahakama kuharakisha kusikiliza na kutoa uamuzi wa kesi zote zinazohusu mauaji ya Shakahola akisema anatumai zitakamilika katika kipindi cha miezi mitatu au sita ijayo ili familia zifarijike na kupata haki.
Kando na hayo ameapa kwamba serikali haitalegeza kamba katika vita dhidi ya mihadarati.
Amesema ‘’Across cutting issue in coast is the problem of drugs and drug abuse and of course we are going to put a lot of emphasis to make sure we tighten our strategies to safeguard our young people and Kenyans of different cadres who are victims of these heinous acts ‘’