Cleophas Malala hatimaye amezungumza baada ya kukamatwa hapo jana.

Katika mahojiano na kituo cha redio moja nchini akiwa katika kituo cha polisi cha Eldama Ravine, Malala ameeleza kusikitishwa na jinsi ambavyo serekali inahangaisha wanafunzi ambao wamejitolea kufunza umma kupitia uigizaji

“We are very disappointed by the manner in which the government is handling this matter. I empathize with the students of Butere Girls who had given out themselves to nurture their talents and expose the evil deeds of this country through art,” Malala alisema

Amedokeza kuwa mchezo huo wa ‘Echoes of war’ imeleta utata kutokana na maudhui yake inayoangazia matakwa ya Gen Zs

“Drama festivals has been there for a long time. It is quite unfortunate for the officials and the administration to victimize young souls who are trying to expose what they think is the rot of our society. I want to call upon everybody in-charge of the drama festivals to sober up! This is just a play and it has got nothing to do with incitement, name-calling.”

“It is a play that talks about the people, exposing the plight of the young generation, popularly the Gen Zs. They are demanding good governance, demanding universal healthcare, accountability and so many other things that they think would paint a good society they want to live in.”

Kuhusu kukamatwa kwake, Malala amedai polisi hawakumweleza sababu ya kutiwa mbaroni akipongeza wanafunzi wa Shule ya upili ya Butere ambao walikataa kuigiza bali walichagua kuimba wimbo wa taifa na kuondoka ukumbini.

“They have told me nothing, I have been behind bars since yesterday 11:00pm. Nobody is talking to me. I’m just in the police cells.”alilia Malala

Malala ambaye ni mwandishi wa mchezo huo alikamatwa hapo jana na hivi sasa ameachiliwa huru.

Kulingana na binamu wake Harry Isiche, Malala ameachiliwa bila mashtaka yoyote kupendekezwa dhidi yake.