Mchekeshaji maarufu nchini Kenya Dem Wa Facebook ameitaja kuwajengea wazazi wake nyumba kuwa hatua kubwa aliyopiga maishani mwake.

Akizungumza na mtangazaji wa Radio 47 Billy Miya na Mbaruk Mwalimu katika kitengo cha ‘Hii si ya kusahau’, mrembo huyo alisisitiza kuwa kuwajengea wazazi ilikuwa ndoto aliyokuwa nayo wakati ambapo alikuwa anazamia tasnia ya ucheshi

“Kitu ambacho sitasahau ni kuaccomplish mission ya kujengea wazazi wangu permanent house,”alianza mcheshi huyo

Alipoulizwa jinsi ambavyo aliufanikisha mradi huo, Dem Wa Facebook alisema hivi, “Ni bidii yangu, kuwork na some brands na nilikuwa nasave doo.”

Amefichua kwamba kitendo hicho kimeongeza thamani yake kwa wazazi wake kiasi wataruhusu aolewe japo shingo upande

Hapo mbeleni katika mahojiano na Ankali Ray, Dem Wa Facebook alidhibitisha kuwa jumba hilo alilowakabidhi rasmi wazazi wake Disemba mwaka jana lilimgharimu takriban shilingi milioni nne

“Nyumba kujenga ilikuwa Ksh 3M, kuweka vitu ndani ilikuwa Ksh 1M”

Pia katika mtandao wake wa YouTube mnamo Januari mwaka huu, aliendelea kukariri kuwa asilimia 99 ya pesa zilizotumika zilikuwa zake wala hakufadhiliwa na watu kama ilivyokuwa ikesemekana mtandaoni

“Kuna mtu alisema eti Dem Wa Facebook alisaidiwa kujenga eti kama hangesaidiwa, hiyo nyumba hangejenga. My dad anajua vile nilikuwa nina struggle. Sikuwa nalala kwa nyumba. Nilikuwa narudi saa sita usiku. What I can say, hiyo nyumba nilijenga with my own money. Support nilipata ile kidogo tu but 99% nilijenga kwa pesa zangu,”alisisitiza

Safari ya mafanikio yake ilianza alipopata nafasi katika kipindi cha Churchill show na baadaye kufanya kazi pamoja na Oga Obinna alipovuma zaidi.

Hivi sasa, umaarufu wake umekuwa mkubwa nchini Kenya na nje ya nchi jambo ambalo limemwezesha kupata matangazo na kampuni za kutaminika.

Pia, amepata tuzo kadhaa kutokana na kazi yake ikiwemo Best Entertainer 2024, Top Facebook Influencer 2024 katika tuzo za Pulse na nyinginezo.