Serikali imepata pigo baada ya Mahakama Kuu kutaja kuwa kinyume na sheria hatua ya Rais William Ruto kubuni jopo-kazi la watu 23 kutathimini maslahi ya maafisa wa polisi.

Katika uamuzi wake mapema Alhamisi, Jaji Lawrence amesema hatua hiyo ya rais kubuni jopo-kazi hilo linayoongozwa na aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga ilikiuka baadhi ya vipengele vya katiba.

Desemba mwaka 2020, Rais William Ruto alibuni jopo-kazi hilo la watu ishirini kutathimini hali ya maslahi na utendakazi wa maafisa wa polisi kote nchini.

Rais Ruto alisema Serikali ya Kitaifa ililenga kuyafanya kipaumbele maslahi ya sekta usalama.

Novemba mwaka 2023, jopo-kazi hilo liliwasilisha ripoti yake ya mwisho kwa rais Ruto katika hafla iliyofanyika katika Ikulu.