Maafisa wa Idara ya Upelelezi DCI wamemkamata Abdirizak Kassim Bare, mshukiwa mkuu wa sakata ya uagizaji wa sukari ambapo wafanyabiashara wanne walipoteza shilingi milioni 100.
Mshukiwa huyo wa umri wa miaka 46, alikamatwa na kuwasilishwa katika Mahakama ya Milimani Jumatano April 9, 2025 baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa hali ya juu uliokuwa ukiendeshwa na DCI dhidi ya kundi la walaghai walioiba fedha zilizotarajiwa kutumika katika ununuzi wa sukari magunia 15, 000.
Katika taarifa, DCI imesema “The investigation established how between May and October 2023, the unsuspecting victims were lured into a business deal to import the sugar, thereby making payments totalling to over a hundred million shillings through five different bank accounts.”
Kilichofuata ni misururu ya misako ya miezi kadhaa dhidi ya washukiwa waliokuwa wametoweka.
Baada ya mchezo huo wa paka na panya washukiwa walijisalimisha katika DCI.
Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma ODPP iliamua mshukiwa kukamatwa na kuwasilishwa mahakamani ambapo alifunguliwa mashtaka manane kukiwapo kujipatia pesa kwa njia ya ulaghai.
Mashukiwa alikana mashata dhidi yake na kuachiliwa kwa bondi ya shilingi milioni 3 ya shilingi nusu milioni pesa taslimu.