Wanandoa mashuhuri Mulamwah na Ruth K wametengana.

Akitangaza rasmi katika mitandao yake ya kijamii, Mulamwah amedhibitisha utengano wao japo hajataja kilichosababisha kuvunjika kwa uhusiano wao.

“Yes, it’s true we have decided to part ways with R.K. It was nice while it lasted,” Mulamwah ameandika katika mtandao wake wa Facebook.

Mwanzoni mwa wiki hii, habari za Mulamwah na Ruth K kusitisha kufuatana katika mtandao wa Instagram iliibuka wengi wakijiuliza iwapo kuna msukosuko kati yao.

Maswali hayo hatimaye yamepata jibu kupitia chapisho hilo la Mulamwah. Hata hivyo, kwa sasa aliyekuwa mpenzi wake Ruth K amesalia kimya kuhusu swala hilo.

Mulamwah mwanzoni alitambulisha Ruth K kwa dunia kama rafiki wake wa dhati kabla ya hatimaye kuweka wazi uhusiano wao.

Baadaye, waliandaa sherehe zao za kimila 29 Oktoba, 2023 kabla ya kufichua kwamba wanatarajia mtoto wao wa kwanza pamoja.

Mnamo tarehe 10 Februari, 2024, wawili hao walitangaza ujio wa mtoto wao kijana Oyando Junior Mulamwah akisherehekea Ruth K kwa kumtunuku zawadi hiyo ya mtoto.

“Welcome to the world, my son. It’s the best feeling in the world… Asante sana Ruth K for this amazing, cute gift. Thanks for always standing by my side. I feel whole again. I feel restored. I am happy; families are now happy; the whole world is happy,” Mulamwah aliandika.

Wamekuwa wakiwapa mashabiki wao picha na video ambazo zimekuwa zikivutia wengi, baadhi wakikiri kutamani kuwa na uhusiano kama yao.

Hivi sasa, wanamitandao wamekuwa na hisia mseto kutokana na kuachana kwao wengi wakiitaja kama kiki ya kupata watu kununua tikiti za kipindi wanaotazamia kuwa nayo Aprili 20, 2025.