Tamasha la Kitaifa la Drama awamu ya mwaka huu, limechukua mkondo ambao hukutarajiwa baada ya wanafunzi wote kususia kuhsiriki ili kuunga mkono Shule ya Upili ya Wasichana ya Butere.
Awali, wanafunzi wa Shule ya Upili ya Wasichana ya Butere waliondoka muda mfupi baada ya kuwasili katika Shule ya Melvin Jones Academy kwa Tamasha la Kitaifa la Drama, mjini Nakuru bila kushiriki.
Wanafunzi hao ambao walitarajiwa kushirikia kupitia mchezo wa kuigiza na ambao umezua utata wa ‘’Echoes of War’’ wameimba tu wimbo wa taifa na kuondoka jukwaani.
Wakizungumza hao wamelalamikia kunyanyaswa kwani wanadai walilazimishwa kushiriki bila watu kushuhudia, mziki, wala jukwaa lililopangwa na kuandaliwa inavyafaa.
Mapema leo maafisa wa polisi waliimarisha doria katia shule hiyo ya Melvin Jones Academy ambapo waliwazuia wanahabari na umma kuingia.
Licha ya shinikizo kutoka kwa vijana waliokuwa miongoni mwa umma kutaka kuruhusiwa kuingia, polisi walitumia vitoza machozi kuwatawanya.
Mchezo huo wa kuingiza ulikuwa umepigwa marufuku lakini Mahakama Kuu mjini Nyamira iliruhusu uwe miongoni mwa ile ambayo ingeshirikishwa katika tamasha hilo.
Cleophas Malala ambaye ni mwandishi wa Mchezo huo anaedelea kuzuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Eldama Ravine baada ya kukamatwa Jumatano jioni.
Malala ameelezea kusikitishwa na hali hii akiitaja kuwa dhuluma kubwa si tu kwa wanafunzi bali pia katika kitengo kizima cha uigizaji.