Waziri wa Madini Ali Hassan Joho amesisitiza ushirikiano wa Chama cha ODM na serikali.
Akihojiwa na Alex Mwakideu na Emmanuel Mwashumbe, katika Breakfast 47 ndani ya Radio 47, Joho amesema kuwa hatua ya ODM kujiunga na serikali ilikuwa kuhakikisha hali ya utulivu nchini na kuwapo kwa mazingira mazuri yanayowezesha maendeleo
Ameendelea kusisitiza kuwa chama cha ODM kinajivunia siasa bora kwa manufaa ya mwananchi, hivyo kujiunga na serikali ilikuwa nafasi ya kutimiza malengo waliyokuwa nayo wakati wa uchaguzi huku wakisaidia serikali ya rais Ruto kuwaongoza wakenya vizuri.
Amesema hivi, “We are here to serve the Kenyan people. To ensure Kenya is stabilized politically, economically and basic standards of life; we enjoy peace and tranquility so that we can create an enabling environment for us to grow. ODM is saying, we don’t have to be playing aggressive politics all the time. There are times where we can sit and say how do we work for the nation? How do we build the nation? For me, we went to an election wanting to form a Government. We had a vision, ambition and ideas. Here came an opportunity to implement the ideas we had and that’s what we are doing today, supporting the Government of President Ruto to do well and serve the Kenyan people.”
Japo hajajibu moja kwa moja iwapo ODM wako serikalini au la, Joho amedokeza kuwa uhusiano wao na Serikali utakuwa wa kudumu hata baada ya mwaka wa 2027.
“Is the relationship temporary or permanent?” aliuliza Mwashumbe
“Kwani wewe ukioa unasema tuoane kidogo?” Waziri Joho akajibu akiongezea kwamba,“ODM is a party and it is entitled to participate in any democratic arrangement. You think ODM is going to die because it joined hands with Ruto? ODM is the biggest stand-alone party today. ODM iko na mpango”
Uhusiano wa ODM na Serikali ya Kenya Kwanza umekuwa ukiibua maswali miongoni mwa wananchi ambao wametaka kujua iwapo bado wapo upinzani au la.