Kukamatwa na baadaye kuachiliwa kwa Cleophas Malala kutokana na mchezo wa Echoes of war kunaendelea kuzua gumzo humu nchini wengi wakitoa hisia zao mseto.
Akizungumza Alhamisi, tarehe 11 Aprili,2025, Waziri wa Elimu Julius Ogamba alieleza kuwa Malala alikamatwa kwa sababu sheria za tamasha za muziki haziruhusu wasio walimu kuongoza na kuwafunza wanafunzi drama shuleni.
“The ministry wishes to inform principals who invite non-teachers to their schools to train learners in co-curricular activities that they are in contravention of the TSC regulations as well as the rules and regulations for the Kenya National Drama and Film Festival.” Alionya Waziri Ogamba.
Tamshi hilo lilichukuliwa kwa uzito ikizingatiwa kuwa Malala amekuwa akiandika na kuwafunza wanafunzi wa shule mbalimbali kwa muda sasa.
Mwanahabari wa Radio 47 Mbaruk Mwalimu aliuliza hivi, “If Malala is not a teacher, is Duale a Doctor?”
“So has Duale treated anyone?” shabiki mmoja akasaili Mbaruk.
“Those asking Why is Malala writing plays for Butere Girls? Are those Text books students using written by their teachers?” Mwengine akajibu.
Ikumbukwe kuwa Duale ambaye amehudumu kama Waziri wa Ulinzi na ambaye hivi sasa ndiye Waziri wa Afya alizamia kozi ya Ualimu katika Chuo Kikuu cha Moi kabla ya kujizolea Uzamili(Masters) katika Utawala wa Biashara Katika Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta.
Cleophas Malala kwa upande mwingine alipata shahada katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Marekani, Afrika (USIU) amekuwa mwanasiasa ambaye amehusika katika kuandika michezo ya kuigiza kwa shule mbalimbali.
Baadhi ya michezo ambazo zimeandikwa na Malala ni The Burdens, Police Brutality, Shackles of Doom Kwa wanafunzi wa shule ya upili ya wasichana ya Butere, Godless iliyoagizwa na wanafunzi wa Riara Springs Academy, Heaven kwa wanafunzi wa shule ya upili ya Mukumu, Echoes of war ambayo imevutia serikali.
Waziri Ogamba alisisitiza kwamba wanafunzi wa Butere hawakuzuiwa kuigiza bali wenyewe waliamua kuondoka ukumbini wakisema hawangeigiza bila mkurugenzi wao Cleophas Malala aliyekamatwa wakati huo.
“The government did not stop Butere Girls from performing. Are you aware that the students were allowed to perform at 8am? When they came to the stage after the National Anthem, one of them said they are not willing to perform without their director, Mr Malala. We cannot allow people to weaponize school children against authority. Let political wars be fought by politicians outside learning environments.”Ogamba aliweka wazi.