Mamlaka Huru ya Uangalizi wa Polisi (IPOA) imeahidi kuchukua hatua dhidi ya maafisa waliodhulumu wanahabari na wanafunzi wakati wa mzozo katika Tamasha za Muziki mjini Nakuru wiki hii.

Machafuko yalizuka Jumatano na Alhamisi wakati polisi waliripotiwa kutumia vitoza machozi kwa wanafunzi wa shule ya upili ya wasichana ya Butere na nguvu zaidi kumkamata mwandishi wa Echoes of War, Cleophas Malala.

Makabiliano hayo yalishuhudia  wanahabari wengine wakipitia dhuluma mikononi mwa maafisa wa polisi wengine wakiondoka na majeraha.

IPOA imedokeza kufahamu malalamishi ya polisi kutumia nguvu ya kupitiliza kwa wananchi, wanahabari na wanafunzi waliohudhuria tamasha hizo wakiahidi kufanya uchunguzi na kuhakikisha polisi waliohusika wanahukumiwa ipasavyo.

“IPOA urges the police to act with professionalism when managing public order. IPOA will continue to monitor the situation closely and carry out impartial investigations. If any officer is found criminally responsible, IPOA will recommend prosecution or disciplinary action,”IPOA imesema katika taarifa maalum.

Huduma ya polisi ya kitaifa (NPS) kwa upande mwingine imedhibitisha kuwa uchunguzi umeanzishwa wakisihi polisi kufanya kazi yao bila kuegemea upande wowote.

“There have been allegations of misconduct by police officers deployed to provide security at the venue. The inspector General of police has instructed the internal Affairs Unit to immediately investigate the matter and present a report within 21 days. Further, the matter is under investigation by the Independent Policing Oversight Authority and other independent bodies. National Police Service reaffirms its commitment to upholding the highest fidelity to the Constitution, operational independence, impartiality and political neutrality in its role of maintaining law and order,” NPS imesisitiza.