Aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua amedokeza kuonekana kwa nadra akinena na wananchi hapa mbeleni.

Akizungumza hii leo katika hafla ya ukumbusho wa Rais wa tatu wa Kenya Mwai Kibaki, Gachagua ametaja kuwa yeye ni mwanafunzi wa kisiasa wa Kibaki, hivyo anajitahidi kufuata nyayo zake.

Kulingana naye, ametaja Kibaki kama Kiongozi aliyefanya mengi kwa maneno machache akidai kwa sasa anaonekana mara moja kwa wiki akiwa na lengo la kuzungumza mara moja tu kwa mwezi.

Amesema hivi, “Mwai Kibaki spoke very little and did much. Most of us are learning from him. Nowadays I only talk once a week. I’m becoming a good student of Mwai Kibaki. Going forward, I’ll talk after two weeks then once a month because he spoke very little and did a lot. I think you don’t need to speak much, you just work and work can be seen.”

Katika hafla hiyo, Gachagua pia amekashifu Serekali kwa kile anataja kama ukatili dhidi ya wanafunzi wa shule ya upili ya Butere.

“We are looking at Butere Girls and unable to understand the viciousness against children by the present government. Even the colonial government spared the children. They have gone berserk and are now fighting shadows, including school girls.”Gachagua alitoa maoni yake

Hivi majuzi, Gachagua ameonekana kuwa na majibizano na Rais Ruto baada ya Rais kudai kwamba alimuitisha shillingi bilioni kumi ili amruhusu kudumu kwa muhula miwili.

Katika kujibu, Gachagua alikana madai hayo akidai kwamba yeye tu ndiye aliweza kuambia Rais Ruto ukweli wakati waliongoza Wakenya pamoja.

“I am now convinced more than ever before, that pathological lying is a mental disorder. The greatest existential threat to our beloved country is outright lying to the people of Kenya without blinking and failure by a leader to put his team together to harmonize their lies. I weep for my Country, Kenya,”alisema Gachagua