‘’Sitamuingiza mke wangu katika siasa’’ ndiyo kauli ya Mbunge wa Emgwen Josses Lelmengit.

Katika mahojiano ya kipekee na Runinga ya TV47 katika kipindi cha ‘’Mfahamu Kiongozi Wako’’ Mbunge huyo amesema ‘’Experienced leaders wakaniambia usimwingize bibi yako kwenye siasa, kwa sababu wewe bado una watoto wadogo na familia changa. Wakae kando wewe endelea na maneno ya siasa na nikafanya hivyo exactly’’

Mbunge huyo ambaye ni miongoni mwa wale wachanga zaidi katika bunge ameelezea changamoto anazokumbana nazo kuilea familia yake changa na kutekeleza kazi zake za uwakilishi wa wananchi.

‘’Jambo la kwanza nilikuja nikasimamisha maneno ya biashara. Biashara yangu ni consitituency because hii ni kama nafanya degree kama tatu…..’’family wamenielewa kwa sababu hata kijana yangu mkubwa sometimes ananiambia Daddy you are going nowhere kwa sababu saa zingine ananipata nimeingia nyumbani saa nne, saa sita natoka asubuhi mapema kabla hajaamka. You find that hata naeza enda wiki moja yote bila kuonana na wao’’

Lelmengit alichaguliwa kupitia chama cha UDA mwaka 2022 akiwa na umri wa miaka 28. Lelmengit alimshinda mshindani wake Tecla Tum, kwa kupata kura 34,803 dhidi ya 13,194 alizopata mshindani wake.