Mcheza Santuri maarufu nchini Kenya DJ Dibul amejitokeza kukana madai ya kukwepa majukumu yake kama baba kwa mtoto aliyebandikiwa.
Kupitia chapisho mbalimbali, uvumi wa DJ Dibul kuhusika kimapenzi na mwanamke aliyetambulishwa kama Agnes ilisambaa mtandaoni.
Baadhi walidai Dibul alitelekeza mwanadada huyo na mtoto wake.
Habari hizo zilimfikia Dibul ambaye ametoa taarifa maalum kutupilia mbali madai hayo.
Kulingana naye, Agnes ni shabiki tu wala hawajawahi kutana tena. Amesema ni hulka yake kupiga picha na mashabiki wake na wakati huu, picha aliyopiga na Agnes imetumika vibaya.
Amerai wanamitandao kuepukana na habari za uongo na kuheshimu familia yake.
“Kuna story nimepata inatrend… eti sijui baby mama, sijui nini…Ni story ya jaba. Ni dem anaitwa Agnes ni fan tu hata hatujawahi patana tena. Mimi naheshimu mafans sana. Huwa napeana selfie so alikuja akachukua selfie. Sasa sijui kama ni yeye alikuwa na intention mbaya ama ni watu wa mitandao waliichukulia the other way..”Ameeleza Dibul.
Agnes kwa upande wake amesihi wanamitandao kusitisha uvumi huo kwani hajawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Dibul.
“Dibul namuonanga tu TikTok. Nilimuona tu once. Watu wanaongea vibaya wachaneni na mimi. For now I’m going through a lot,” amesema akifichua kupata habari hii akiwa kazini.
DJ Dibul na mpenzi wake Dorea Chege walikaribisha mtoto wao tarehe 24 Machi, 2025.
Kupitia chapisho na matamshi yake katika mitandao ya kijamii, Dibul ameweka wazi kufurahia kuwa baba wakati mmoja akisema,”Nashangaa wenye hawana watoto mnaishingi aje kwa hii life.”