Rais William Ruto amemshukuru Kiongozi wa ODM Raila Odinga kwa kusimama na kukubali kushirikiana naye wakati akikabiliwa na hali ngumu katika uongozi wake.
Akizungumza wakati wa hafla ya mazishi ya aliyekuwa Mlinzi wa Raila George Oduor katika Kaunti ya Siaya Jumamosi, Rais amesema Raila amesimama naye jinsi alivyofanya wakati wa kipindi kigumu cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.
Rais amesema hivi, ‘’ I am truly greatful that just the same way I stood with you when you needed a nab ti stand with you, you have equally come to stand with me when I needed a man to stand with me’’
Kulingana na Rais, Raila ameonesha uzalendo mkubwa kwani alifanya hivyo kwa manufaa ya nchi wala si ya kibinafsi ‘’ When Baba here came to stand with me, it was not about him, it was not about his interests., It was about the greater interest of Kenya and history is going to judge the honorable Raila Odinga fairly’’ Alisema Rais.
Rais amesema upo uwezekano wa kila mmoja kunufaika bila kuzua migawanyiko akisema ”Nani alisema kuna watu walipangiwa kukaa nje ya serikali kila wakati?”
Akionekana kumlenga Rigathi Gachagua Rais amesema hatakubali tena ukabila na ubaguzi kuenea nchini akisema kuna haja ya ushirikiano kwa manufaa ya wananchi wote.