Rais William Ruto ni miongoni mwa viongozi wanaohudhuria hafla ya mazishi ya aliyekuwa mlinzi wa Raila Odinga, George Oduor.
Hafla hiyo inaendelea mjini Ndori, Siaya katika Uwanja wa Shule ya Msingi ya Ramba.
Miongoni mwa viongozi ambao tayari wamewasili katika hafla hiyo ya mzishi ni Waziri wa Kawi Opiyo Wandayi, Magavana James Orengo wa Siaya, Gladys Wanga wa Homa Bay, Anyang’ Nyong’o wa Kisumu , Ochillo Ayacko wa Migori wabunge na viongozi wengine.
Oduor amekuwa mlinzi wa Raila kwa muda mrefu tangu miaka ya tisini. Alifariki dunia Machi tarehe 3, alipokuwa akitibiwa katika Hospitali ya Nairobi West jijini Nairobi.