Washukiwa wa wizi wa mifugo wanaoaminika kutoka Pokot Kaskazini wamekivamia kijiji cha Nakalimon katika eneo la Loima, Kaunti ya Turkana, na kuiba ng’ombe 114.

Wakati wa tukio hilo, mvulana mmoja mwenye umri wa miaka 18, alipigwa risasi na kujeruhiwa sehemu ya chini ya mgongo. Kwa sasa anaendelea kutibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Lodwar na hali yake inaendelea kuimarika.

Aidha maafisa wa Usalama wamefanikiwa kuwapata ng’ombe 106 katika eneo la Nayakori, umbali wa kilomita tano kutoka Pokot Kaskazini.

Ng’ombe wanane bado hawajapatikana.

Polisi wanaendeleza msako na hali ya kawaida imerejea katika eneo hilo.