Mwili wa Yusuf Ali Abdi aliyefukiwa katika vifusi vya jengo hatari la ghorofa 11 Mombasa hatimaye umepatikana.

Akizungumza leo hii tarehe 13 Aprili, 2025, Gavana wa Mombasa Abdullswamad Sheriff Nassir amedhibitisha habari hii akishukuru familia na kaunti kwa kushirikiana kufanikisha kupatikana kwa mwili huo.

“Through the close collaboration of the bereaved family and the tireless efforts of our county teams—who have worked around the clock for the past three days—we confirm the recovery of the body of Yusuf Ali Abdi. We are grateful to everyone who played a part in this difficult and emotional operation.” Governor Nassir ameandika katika mitandao yake wa kijamii.

Akituma rambirambi zake kwa familia, Gavana Nassir ametoa ombi kwa wanahabari kutoa habari inavyostahili akidai kwamba wanahabari wengine waliiweka kana kwamba jumba hilo lilibomolewa wakati mwendazake alikuwa akiingia.

Mnamo Aprili 2, 2025, Yusuf Ali Abdi aliingia katika jengo hilo la ghorofa 11 lililokuwa likijengwa katika eneo la Kilifi Corner la Fayaz Estate kando ya Barabara ya Abdel Nasser huko Mombasa kukagua kitengo alichokusudia kununua.

Alikuwa ametoka tu kwenye msikiti wa karibu baada ya sala za jioni. Dakika chache baada ya kuingia kwenye jengo hilo, inadaiwa alinaswa wakati ilianguka. Hiyo ilikuwa mara ya mwisho kwa mfanyabiashara huyo wa Soko la Marikiti kuonekana akiwa hai, kulingana na picha za CCTV.

Hapo awali, familia yake ilishuku kuwa alikuwa ametekwa nyara na kutafuta msaada kutoka kwa kikundi cha Waislamu wa Haki za Binadamu (Muhuri). Hata walifanya maandamano katika Soko la Marikiti, wakidai mpendwa wao alikuwa ametoweka chini ya hali isiyoeleweka.

Siku sita baadaye, picha za CCTV ziliibuka zikithibitisha kwamba alikuwa amenaswa kwenye jengo lililoanguka, na kuiacha familia na maswali mengi kuliko majibu.

Waliarifiwa kuwa ilikuwa hatari sana kuitoa mwili wakati huo na hivyo walilazimika kusubiri Jeshi la Ulinzi la Kenya(KDF) kuangusha muundo huo mbaya. Serikali ya kaunti tangu wakati huo imekuwa ikiondoa fusi(debris) kutafuta mabaki yake.

Familia yake imekuwa ikipiga kambi kwenye eneo la jumba hilo, ambalo liliangushwa na KDF mnamo Aprili 9, 2025.

Baada ya kupatikana kwa mwili wake, Liban Hassan ambaye ni ndugu yake na  msemaji wa familia ameshukuru Serikali ya Kaunti ya Mombasa, wanahabari na Wakenya kwa kuwasaidia kwa njia tofauti tofauti katika kipindi kilichokuwa kigumu cha kutafuta mpendwa wao.

Gavana Nassir amesema mtu mmoja ameachishwa kazi na mwengine kutumwa kwa likizo la lazima kufuatia ujenzi wa jengo hilo ambalo liliweka maisha ya wengi hatarini.