Mhubiri maarufu nchini Kenya James Maina Ng’ang’a amejipata pabaya baada ya video moja akizaba mwanaume mmoja makofi kwa kosa la kulala kanisani kusambaa mtandaoni.

Katika video hiyo ya takriban dakika moja na sekunde ishirini na sita iliyonasa macho ya wengi, Ng’ang’a alizaba mshirika huyo makofi na kumuamuru aende akae nyuma kabla ya kugeukia aliyekaa kando yako.

“Me I hate drama,I swear before God. Unaona sasa, Kenya iko mambo mengi sana, Amka!..Amka! Enda nyuma…Kwenda huko st*pid. You just tell me, hivi nimechacha hivi na mtu amelala. Hivi nimekasirika hivi na mtu amelala na amekaa kiti ya mbele,” Ng’anga alisema huku akimzaba mwanaume huyo makofi

Mbunge wa Homa Bay Mjini Peter Kaluma aliyepata kutazama video hiyo amekashifu Ng’ang’a akiomba mamlaka husika kumkamata na kumfungulia mashtaka.

Kulingana naye, mhubiri huyo anafaa atiwe mbaroni kabla ya mabaya zaidi kutokea.

Kaluma ameandika hivi,“Ng’ang’a must be arrested, prosecuted and jailed before worse happens at Neno Evangelism.”

Vilevile, ameitisha msaada wa umma kwa yeyote anayefahamu mwanaume aliyedhulumiwa na Ng’ang’a katika video hiyo kuripoti kwa polisi ama kwake ili hatua zinazofaa zichukuliwe.ll

“Whoever knows the guy he is assaulting in this video or any of the many worshippers he has ever assaulted should report to the nearest Police Station or see me immediately for urgent action.”

Kaluma pia amesihi msajili wa vyama kufuta usajili wa Kanisa la Neno Evangelism mara moja.

Si mara ya kwanza Ng’ang’a anatrend mtandaoni. Mnamo January 29, 2025, Ng’ang’a alijipata katika vichwa vya habari baada ya kushauri mwanamke, Milka Tegesi, aliyemletea malalamishi ya kufungiwa nyumba kuenda kuishi kwa nyumba za bei nafuu (affordable houses)zinazojengwa na serekali.

“Pastor nimefungiwa nyumba one week…”Tegesi alililia Ng’ang’a

“Enda polisi! Si kuna nyumba zimejengwa zinaitwa affordable. Enda ukae kwa hizo. Shida ya nyumba usiniletee enda kwa Government. Hapa ni kwa maombi, pesa enda kwa Sakaja. I deal with spiritual matters mambo kuhusu pesa don’t come here expecting money, I don’t give money,”Ng’ang’a alimjibu na kuzua gumzo mtandaoni.

Tegesi alipata msaada mkononi mwa afisa Sammy Ondimu Ngare ambaye alihakikisha amepata kazi, simu mpya na hela za kuendelea na maisha yake.