Idra ya Huduma za Polisi NPS imesema imepokea barua ilyoandiskwa na aliyekuwa Naibu Rais, Rigathi Gachagua, akilalamikia kutopewa ulinzi na polisi. Katika barua hiyo, Gachagua anadai kuwa maisha yake na ya familia yake yamo hatarini kutokana na kile anachokitaja kuwa ni mpango wa makusudi wa kumdhuru, akiwahusisha maafisa wa polisi, magenge ya wahalifu, na maafisa wa ujasusi katika njama hiyo.
Katika Barua kupitia Msemaji wa Idara ya polisi Muchiri Nyaga ni kwamba Inspekta Jenerali wa Polisi anasisitiza idara hiyo ina jukumu muhimu katika kuendeleza na kulinda usalama wa taifa na kuhakikisha usalama wa wakenya wote.
Kuhusu wasiwasi kufuatia usalama wake, Gachagua, anashauriwa kushirikiana na maafisa wa polisi katika ngazi zote iwapo atahitaji hatua za ziada za usalama, na kuwajulisha polisi mapema kuhusu harakati na shughuli zake za umma ili kuwezesha mipango ya ulinzi wake.
NPS imeihakikishia umma kuwa hali ya usalama nchini kote i thabiti, na hatua za tahadhari zimechukuliwa ili kuzuia uhalifu wa aina yoyote.
Katika taarifa hiyo Nyaga amesema Idara hiyo haina mapendekeo yoyote ya kisiasa.
Mapema Jumanne, Gachagua amemwandikia Inspekta Mkuu wa polisi Douglas Kanja akidai kuwapo kwa njama za kutaka kumuua.