Kampuni ya mabasi ya uchukuzi wa umma Super Metro imesitisha shughuli zake kwa muda wa siku tatu ili kutoa nafasi ya kutekeleza matakwa yote ya kisheria.
Kampuni hiyo, kupitia taarifa iliyotolewa Jumatatu, ilisema kuwa Bodi ya Rufaa ya Leseni za Usafiri (TLAB) imeiagiza kusitisha shughuli zake kwa muda wa siku tatu ili kukamilisha hatua zilizobaki za kutii masharti.
Kwa mujibu wa Super Metro, tayari imetekeleza asilimia 90 ya masharti yaliyotolewa na Mamlaka ya Kitaifa ya Usafiri na Usalama Barabarani (NTSA) pamoja na Bodi ya Rufaa ya Leseni za Usafiri (TLAB).
Katika kutangaza hatua hiyo, kampuni ilieleza kuwa itaheshimu maamuzi ya TLAB na mahakama, na ikaongeza kuwa itafanya kazi kwa bidii kushughulikia masuala yaliyosalia ya kutii masharti ndani ya muda uliowekwa.
Imesema hivi “Following a hearing with the Transport Licensing Appeals Board today, the Board has directed Super Metro Limited to suspend operations for the next three days to finalise the remaining compliance measures,” Super Metro announced.
“Super Metro Limited fully respects the decisions of the TLAB and the court. We are working diligently to address the outstanding compliance issues within the stipulated timeframe and will resume operations as soon as we receive approval from the relevant authorities,” it added.

Kampuni hiyo imewaomba msamaha wateja na washikadau kwa usumbufu ambao kusitishwa kwa shughuli kwa muda kutasababisha, lakini ikaahidi kuendeleza utoaji wa huduma za usafiri zilizo salama, za kuaminika, na zenye ufanisi. Tangazo hili la hivi punde linajiri mwezi mmoja baada ya TLAB kuondoa marufuku kwa muda ya kuhudumu iliyokuwa imetolewa na Mamlaka ya Uchukuzi na Usalama Barabarani hadi suala hilo litakaposikilizwa na kuamuliwa.
Ikumbukwe Machi 20, NTSA ilitangaza kusitisha leseni ya kuhudumu ya Super Metro kufuatia kile ilichotaja kuwa kutofuata sharia za huduma za uchukuzi wa umma.