Waziri Mteule wa Jinsia, Hanna Cheptumo, ameomba msamaha kufuatia kauli yake tata kuhusu mauaji ya wanawake aliyoitoa wakati wa mchujo wake, akisema anawajibika kikamilifu na kujitolea kulinda haki na maisha ya wanawake nchini Kenya.
Cheptumo, ambaye aliidhinishwa na Bunge Jumatano, alisema kauli yake ilikuwa ya kusikitisha na haikuakisi imani wala nia yake.
Alisema hivi, “In the course of my interview, I made a comment in response to a question on the murder of women in AirBnBs. I would like to take this opportunity to take accountability for this statement and to clarify my position.”
Wakati wa mchujo , Cheptumo alikosolewa vikali na umma baada ya kuonekana kupuuza ongezeko la visa vya mauaji ya wanawake vinavyoripotiwa kote nchini katika miezi ya hivi karibuni. Kauli yake ilizua hisia kali miongoni mwa makundi ya kijamii na wanaharakati wa haki za wanawake waliotaka aombe msamaha na kurekebisha kauli hiyo.
Jumanne, Cheptumo aliahidi kuwa mstari wa mbele katika vita dhidi ya ukatili wa kijinsia (GBV), akieleza kuwa moja ya vipaumbele vyake kama Waziri wa Jinsia iwapo angeidhinishwa ni kuimarisha mifumo ya ulinzi kwa wanawake na wasichana.
Alisema, “I commit to working with all stakeholders to ensure we create a safer Kenya for women. I will lead this fight from the front.”
Kupitishwa kwake na Bunge sasa kunafungua njia kwa uteuzi rasmi kutoka kwa Rais William Ruto.