Rais William Ruto ameapa kukilinda Kikosi cha Ulinzi cha Kenya (KDF) kwa njia zote zinazowezekana, huku akionya dhidi ya juhudi za kulichafulia jina jeshi hilo, kufuatia hatua ya baadhi ya viongozi wa upinzani kuibua maswali kuhusu matokeo ya uchunguzi wa ajali ya helikopta iliyosababisha kifo cha Jenerali Francis Ogolla.
Ruto amewataka Wakenya kushuyaghulikia masuala ya usalama wa taifa kwa umakini mkubwa.
Akizungumza katika hafla ya kufuzu kwa maafisa wa kadeti katika Chuo cha Kijeshi cha Kenya (Kenya Military Academy) kilichoko Lanet, Kaunti ya Nakuru, Rais ametangaza kuwa serikali itatetea heshima na uadilifu wa jeshi, ambalo alilitaja kuwa msingi wa amani, uthabiti, na maendeleo ya taifa.
Amesema, “The government will defend the military by all means possible,” “They are the guarantors of our stability and development.”
Kulingana na Rais usalama wa kweli ni jukumu la pamoja, na kila raia ni mshirika. Amewasihi viongozi, wanasiasa, vyombo vya habari, na umma kwa ujumla kuwa na tahadhari wanapojadili masuala yanayohusu jeshi.

Rais pia alifichua kuwa kuna mabadiliko yanaoendelea ili kuliboresha jeshi la KDF, kukiwamo kulinganisha mafunzo yake na mikakati ya kisasa ili kukabili vitisho vipya vya kiusalama kama vile vita vya kidijitali, uhalifu wa kimataifa, na mbinu zisizo za kawaida za kivita.
Alisema, “In response, we must modernise our forces, tailor our training, and innovate and update our doctrine.”
Hafla hiyo ya Jumatano pia iliandikisha historia kwa kuliapisha kundi la kwanza la kadeti waliomaliza masomo na kupata Shahada ya Kwanza katika Masuala ya Ulinzi na Usalama kutoka Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Ulinzi chaKenya.
Rais alisema, “Through these efforts, KDF remains a bulwark of peace and stability not only in Kenya, but also in the region and across Africa.”
Waliohitimu walijumuisha maafisa kutoka Burkina Faso, Msumbiji, Rwanda, Sierra Leone, Tanzania, na Uganda hatua ambayo Rais alitaja kuwa ishara ya ushirikiano unaokua katika ukanda wa Afrika kuhusu masuala ya ulinzi.