Shinikizo limezidi kwa mwanaye marehemu Mbunge wa Malava, Malulu Injendi, kutangaza azma ya kumrithi babake na kukamilisha miradi ya maendeleo aliyoanzisha.
Rhyan Injendi, ambaye ni mwanaye wa kwanza wa marehemu, ameashiria kuwa atawania kiti hicho cha ubunge wakati mwafaka utakapowadia.
Akizungumza wakati wa hafla ya kumbukumbu ya marehemu iliyofanyika nyumbani kwao katika eneo la Lugusi, Malava, Rhyan alikubali wito wa kuwania ubunge wa Malava kwa muda uliosalia wa miaka miwili. Hotuba yake ya kukubali ilipokelewa kwa nderemo na vifijo kutoka kwa umati uliomheshimu kama mgombea anayeungwa mkono zaidi kuliko wengine waliotangaza nia.
Sherehe hiyo iliyoongozwa na Parokia ya Kanisa Katoliki ia Malava chini ya uongozi wa Padre Vincent Sanga, iliangazia kumbukumbu ya maisha ya kiongozi huyo aliyetajwa kama mtu wa amani na aliyejikita kwenye maendeleo, atakayekumbukwa na wengi.
Ni wakati wa sherehe hiyo Rhyan alitangaza hilo, akisema kuwa baba yake aliacha miradi mingi ya maendeleo ambayo inahitaji kukamilishwa, na kuwa haitakuwa sawa kwa familia, kwa heshima ya baba yao, na kwa eneo hilo kwa jumla iwapo hatakubali kuendeleza uongozi huo wa kisiasa.
Kauli hizo zilipokelewa kwa furaha tele huku wafuasi wa marehemu wakimsifu kwa kuchukua uamuzi huo wa kishujaa kuwaongoza.
Aliwashukuru viongozi wa kisiasa wakiongozwa na Rais William Ruto, marafiki, familia na watu wa Malava kwa kusimama na familia yao wakati wa majonzi, na kupongeza mshikamano wao wa kumpa marehemu mazishi ya heshima.
He requested, “Your unity and support you showed us during our time of grief is a clear indication that you not only believed but trusted our father as a true leader and for the Malava people thank you for trusting in him and electing him to serve you for three terms starting 2013, 2017 and 2022 and he was still working to ensure that Malava becomes developed but he left before he could accomplish his goal of bettering the constituency and that is why I’m humbly asking for your support to steer me to parliament to complete what my father started.”
Alisema amekuwa akipokea simu na maombi kutoka kwa umma na wafuasi wa baba yake wakimtaka achukue nafasi hiyo, na kwamba shinikizo hilo limekuwa kubwa kiasi cha kumlazimu kukubali.
Aliongeza kuwa anasubiri Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuundwa na kuanza kazi, kisha serikali itatangaza kiti hicho kuwa wazi, na kufungua njia kwa uchaguzi mdogo.
He noted, “I am aware that my father left some projects including infrastructure such as roads, KMTC, electricity and security pending and which I feel obligated to complete them on his behalf if you give me that chance to do so considering that its only two years remaining to the next polls, I want to be the one to complete them and as for 2027 we will cross that bridge when the right time comes but for now I’m concerned about finish what our Mp started.”
Awali, wakati wa mazishi ya marehemu, Katibu Mkuu wa COTU, Francis Atwoli, aliitaka familia impe serikali mmoja wa wana wanne wa marehemu kuchukua nafasi hiyo na kukamilisha miradi ya maendeleo iliyoanzishwa na baba yao.
Wakati uo huo, msaidizi wa Rais William Ruto, Farouk Kibet, pia alisisitiza kuwa serikali ya Kenya Kwanza haitaruhusu kiti hicho kuchukuliwa na upinzani kwani marehemu alikuwa upande wa serikali.
Hadi sasa, wagombea 31 tayari wametangaza nia ya kuwania kiti cha eneobunge la Malava.