Hatimaye serikali imevunja kimya chake wiki moja baada ya tukio la kushangaza ambapo wanafunzi wa Shule ya Upili ya Wasichana ya Butere walirushiwa vitoza machozi katika Tamasha la Kitaifa la Drama huko Nakuru.

Mkuu wa Kitengo cah Ubunifu na Miradi Maalum katika Ikulu ya Rais Denis Itumbi amewaomba msamaha wasichana wa Shule ya Upili ya Butere akisema serikali ”Iliwaangusha”.

Akiwa kwenye Runinga ya Citizen Jumatano usiku, Itumbi alikiri wazi kwa niaba ya serikali na kuwaomba msamaha wanafunzi pamoja na washikadau wote wa Shule hiyo ya Butere kufuatia kilichotokea.

Kauli yake, iliyotolewa kwa sauti ya huzuni na uwazi, ilikuwa ni mara ya kwanza kwa afisa wa ngazi ya juu wa serikali kukiri hadharani kuhusu tukio hilo la kusikitisha ambalo limekuwa gumzo kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Itumbi alisema, “Let me take this opportunity, with the full sleeves and honors of the government, to apologize to all the girls of Butere Girls for the teargas that was fired at them. I sincerely apologize.”

Alikiri kuwa serikali ilishindwa kuwalinda wanafunzi hao na pia haikushughulikia hali hiyo ipasavyo, jambo ambalo liliwanyima nafasi ya kuigiza mchezo wao wa Echoes of War katika jukwaa la kitaifa onyesho ambalo walikuwa wamejiandaa nalo kwa miezi kadhaa.


“We are not only sorry for the teargas but also for not managing this to the very end,” Itumbi added. “I promise to sit down with my team and come up with remedies for what can be done.”

Akiwa kama afisa anayeongoz Ubunifu, kauli ya Itumbi ilibeba uzito mkubwa. Msamaha wake haukuonekana kuwa wa kibinafsi tu bali pia wa taasisi nzima ya serikali kukiri kwamba mfumo umeshindwa kulinda sanaa, vijana, na uhuru wa kujieleza kwa wakati mmoja.

Aliweka bayana pia kuwa kuna uvumi unaosambaa kuhusu adhabu dhidi ya Mwalimu Mkuu wa shule hiyo na walimu wa drama haukuwa na msingi.


“If my facts are correct, the principal at Butere Girls is actually going to retire sometime this year, in two months. She has had a stirring career as a teacher, and we will allow her to finish her call of duty,” alifafanua

Itumbi, ambaye pia alifichua kuwa yeye ni mwandishi wa tamthilia, alielezea kuvutiwa kwake na ujasiri na ari ya wasichana hao kwa sanaa ya maigizo, na kusisitiza kwamba onyesho lao ambalo halikusikika limeanzisha mjadala wa kitaifa ambao unapaswa kuleta mabadiliko ya kimuundo katika namna wanafunzi wasanii wanavyotendewa.


Itumbi ameomba msamaha huo kufuatia matukio ya kusikitisha ya Aprili 9, ambapo Wanafunzi wa Shule hiyo ya Butere walikuwa walihangaishwa wakati wa kuigiza mchezo wao Echoes of War katika Tamasha la Kitaifa la Drama, walipojikuta hawana vifaa muhimu, vifaa vya a sauti (PA system), na muhimu zaidi, mwongozaji wao ambaye ni aliyekuwa Seneta Cleophas Malala aliyekamatwa siku moja kabla ya maigizo.

Kwa ishara ya kupinga yaliyotokea, wanafunzi waliimba wimbo wa taifa na wakaondoka jukwaani, hatua iliyotafsiriwa na wengi kama kitendo cha heshima na ujasiri.