Kufuatia ripoti za hivi ounde za vyombo vya habari kuhusu visa vya biashara haramu ya viungo vya binadamu, Serikali ya Israeli imeapa kupambana kimataifa na uhalifu huo wa kikatili.

Israeli imesema ilitia saini Azimio la Istanbul kuhusu Biashara ya Viungo na Utalii wa Upandikizaji, na inasimama imara katika kutekeleza misingi ya azimio hilo.

Kupitia taarifa kutoka kwa ubalozi wake, Israel imesema inalaani vikali aina zote za biashara haramu za viungo na vitendo vingine visivyo halali vinavyohatarisha maisha na heshima ya wanaotoa na wanaopokea viungo hivyo.

Imesema vyombo vya usalama vya Israeli vinaendelea kuwa makini katika kupambana na biashara hiyo haramu, na kwa kushirikiana na washirika wa kimataifa. Taarifa hiyo imesema uhalifu huo unachukuliwa kwa uzito mkubwa, na hatua za kisheria huchukuliwa ipasavyo dhidi ya wanaohusika.

”We believe and hope that all such illegal acts will be thoroughly investigated and appropriately addressed by the relevant authorities.

The Embassy of Israel remains available to cooperate and provide any assistance necessary in clarifying facts or supporting efforts to combat organ trafficking.” Ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hii inajiri baada ya Kenya kusitisha huduma za ubandikizaji wa figo katika hospitali ya Medheal iliyoko Eldoret.

Hospitali ya Medheal imehusishwa na ulanguzi wa viungo vya binadamu katika ripoti iliyotolewa Jumanne na Wizara ya Afya. Hata hivyo, hospitali hiyo imejitetea na kupinga taarifa hiyo