Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi DCI Mohamed Amin amemuonya Naibu Rais wa zamani Rigathi Gachagua dhidi ya kuingilia masuala nyeti ya usalama.

Akiwahutubia wanahabari Jumamosi, Aprili 19, mkuu huyo wa DCI amemkemea vikali Gachagua akisema anazua vitimbi mbele ya vyombo vya habari kuhusu mhumimu ya usalama.

Akijibu madai ya hivi karibuni ya Gachagua kuhusu jaribio la kutaka kumuua, Amin amemshauri Naibu huyo wa Rais aliyetimuliwa madarakani kufuata njia rasmi za kisheria kwa kuripoti suala hilo katika kituo cha polisi kilicho karibu naye.

Amin amesema kuwa, kama ilivyo kwa kila raia wa Kenya, Gachagua atapata ulinzi anaohitaji ili kuhakikisha usalama wake na wa mali yake unalindwa.


Amin ameeleza, “If the former Deputy President has an issue in matters concerning the threat to his life and property, he should go and report to the nearest police station and stop engaging in media theatrics.”

Kulingana na Amin taarifa yoyote, kama ilivyo kwa wananchi wengine hii, itachunguzwa hadi kufikia hitimisho la kimantiki. Akifafanua ,I associate myself fully with the sentiments of the Inspector General and encourage Gachagua to report the matter to his nearest police station.” 

Kauli za Mohamed Amin imejiri siku nne tu baada ya Gachagua kupaza sauti kuhusu madai ya njama ya kumuua na vitisho vinavyoendelea dhidi yake na familia yake.

Katika taarifa aliyomwandikia Ispekta Mkuu wa Polisi Douglas Kanja Jumanne, Aprili 15, Gachagua alitaka polisi wachukue hatua za haraka kumuimarishia usalama, familia yake na mali zake.

Gachagua alimshtumu Kanja kwa kile alichodai ni hatua ya kumpokonya ulinzi makusudi, akisema ni njama ya kumweka hatarini.

Gachagua pia alidai kuwa maafisa kutoka Idara ya Ujasusi wa Kitaifa NIS walikiuka haki yake na kumfuatilia pamoja na familia yake kwa kutumia magari yasiyotambulika.