Mwakilishi Wadi wa Kariobangi North Kaskazini Munuve amefariki dunia.
Spika wa Bunge Kennedy Ngondi amesema Munuve, amezirai ghafla mapema leo na kufariki alipokuwa akitibiwa katika Hospitali moja ya kibinafsi iliyoko katika Barabara ya Kiambu.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari Ngondi amemtaka marehemu Munuve kuwa kiongozi aliyejitolea katiaka kazi yake.
Amesema kifo hicho ya ghafla ni pigo si tu kwa familia yake bali kwa Wakazi wa Kariabangi Kaskazini na Bunge la Kaunti. Ngondi amesema mipango ya mazishi itatangazwa baadaye.