Aliyekuwa mgombea wa urais mara mbili Mwalimu Mohammed Abduba Did, ameachiliwa kutoka gerezani nchini Marekani baada ya kuhudumia kifungo cha miaka mitatu.

Dida alipaswa kuachiliwa kutoka gerezani Aprili 3, mwaka 2029 baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka saba, hata hivyo ameachiliwa kwa msamaha.

Kulingana na rekodi kutoka kwa gereza la Big Muddy Correctional Facility lilikoko Jimbo la Illinois, Mwalimu Dida aliachiliwa huru Machi, 3 hivyo atafanya kazi ya jamii katika muda wa kifungo uliosalia nchini Marekani.

Dida alifungwa gerezani tangu Novemba 18, mwaka 2022 baada ya kupatikana na hatia ya kumwandama na kumtishia mkewe Mmarekani.

Katika stakabadhi za mahakama Dida alipatikana na hatia ya kukiuka maagizo ya kumzuia kuingia eneo alilokatazwa na mahakama jambo ambalo ni kinyume na sheria za Marekani.

Tukio hilo lilifanyika wakati Dida alipoenda msikiti uliokaribu na mkewe huyo. Jabo ilibainika kwamba nia yake ilikuwa ni kuhudhuria sala, hatua kwamba msikiti ulikuwa katika eneo alilokatazwa kwenda basi iliwalazimu walinda usalama kumkamata na kumzuilia.

Mmoja wa jamaa yake alisema hivi “He went to a mosque nearby to pray, not knowing it was within an area he was barred from entering, as Mama Lila also frequently visited the same mosque.”

Familia ya Dida inasema hatua yake kukiuka agizo hilo haikuwa ya maksudi hivyo wanaiomba serikali kumsaidia na hatua zote za kisheria.

Kabla ya kuhukumiwa nchini Marekani Dida alikuwa akifanya kazi na shirika moja lisilo la kiserikali ambalo huduma zake ni za kuzisaidia jamii ambazo hazijiwezi nchini Marekani na Afrika.

Shirika hilo la Dida Foundation International, lililoko Minneapolis, lilisajiliwa mwaka 2019