Waziri wa Elimu Julius Ogamba amefafanua kwamba Hisabati itaendelea kuwa somo la lazima katika shule za msingi na sekondari.
Kwa mujibu wa Ogamba, hatua hii inafuatia mashauriano ya kina na washikadau ambapo pendekezo la kuifanya kuwa somo la hiari lilitupiliwa mbali.
Hata hivyo, alionyesha kwamba wanafunzi wa sanaa watafundishwa toleo la kiurahisi la Hisabati.
Alisema “The majority of stakeholders during the CBC dialogue were of the view that mathematics should be compulsory in senior school. We have listened to your concerns, consulted with the Kenya Institute of Curriculum Development (KICD), and resolved that some form of mathematics be made compulsory for the two pathways that are not STEM.”
Maafikiano haya yametokana na alalamiko kuhusu pendekezo la kufanya Hisabati kuwa somo la hiari, ambapo Chama cha Walimu wa Shule za Upili na Vyuo vya Kadri KUPPET kilikosoa hatua hiyo, kikisema itadororesha viwango vya elimu.
Ikumbukwe Wizara ya Elimu ilitangaza kuwa Hisabati haitakuwa ya lazima kwa wanafunzi wa sekondari chini ya Mfumo wa Mitaala wa Umilisi CBC.
Katika mfumo huo, wanafunzi walikuwa wakichagua masomo manne ya lazima, yaani Kiingereza au Lugha ya Ishara ya Kenya, Kiswahili, Michezo na Huduma kwa Jamii. Kisha wangechagua masomo mengine matatu kutoka kwa orodha ya mengine 8.