Kwa mara ya kwanza katika historia ya Marekani idadi ya wanawake wanaopata watoto wakiwa na umri wa miaka arubaini na zaidi imezidi ile wa wasichana waliobalehe teens.
Takwimu hizi ni kulingana na utafiti uliofanywa na Kituo cha Kuthibiti Maambukizi ya Magonjwa cha Marekani CDC.
Katika utafiti huo, takwimu hizi zinaashiria hatua ya wanawake wengi wa kuamua kutopata watoto au kusubiri hadi baadaye katika maisha.
Sio hayo tu, kwa mara ya kwanza Marekani imerekodi idadi ya chini ya watoto wanaozaliwa kulinganishwa na miaka ya nyuma.
Utafiti huo unaonesha kuwa idadi hiyo imepungua kwa asilimia 14% kati ya mwaka 1990 na mwaka 2023.
Katika kipindi hicho, viwango vya uzazi miongoni mwa wasichana walio na umri chini ya umri wa miaka 20 vilipungua kwa asilimia 37%, ikiwa ndiyo asilimia kubwa zaidi ya upungufu miongoni mwa makundi yote ya umri.
Aidha idadi ya wanawake wa kati ya umri wa miaka 20 na 24 waliojifungua ilipungua kati ya mwaka 1990 na 2023. Aidha idadi ya wanawake wa kati ya umri wa miaka 25 na 29 wanaojifungua ilipungua kwa asilimia 23%.
Utafiti huo unaonesha idadi ya wanawake wa kati ya umri wa miaka 30 na 34 waliojifungua iliongezeka kwa asilimia 24% huku wale wa kati ya umri wa miaka 34 na 39 waliojifungua katika kipindi hicho iliongezeka kwa asilimia 90%.
Wanawake wa umri wa miaka 40 wanaojifungua waliongezeka kwa silimia 193% katika kipindi hicho.
Katika miaka ya tisini asilimia 69.8% ya wanawake wa chini ya umri wa miaka 30 walikuwa wakijifungua.
Sehemu ya ripoti hiyo ilisema hivi, “The magnitude of the decrease in birth rates among females younger than 30 was greater than the magnitude of the increase in rates among women 30 and older, resulting in declining overall fertility rates.”
Wataalam wa afya wamesema hali hii imetokana na sababu mbalimbali zikiwamo kuimarika kwa huduma za afya ya uzazi kwani kutokana na teknolojia wanawake wana uwezo wa kusubiri hadi baadaye ili kupata watoto.
Kando na hilo matatizo ya kifedha yamewafanya wengi kuchagua kutopata watoto.