Mvua kubwa inayoendelea kunyesha ikiandamana na upepo mkali imewaacha wakazi na hasara kubwa huku baadhi ya shule na nyumba zikibomoka eneo la Kotinyang’ katika wadi ya Katilu, Kaunti ndogo ya Turkana Kusini.
Mvua hiyo ambayo ilianza siku ya Jumatano imesababisha Shule ya Msingi ya Korinyang’ iliyo na idadi ya wanafunzi zaidi ya elfu mbili, kukosa kufunguliwa wiki ijayo, baada ya mvua ya radi iliyokuwa imeandamana na dhoruba kung’oa paa zote za Madarasa na kuharibu kuta za shule hiyo siku ya Jumatano.
Mwalimu mkuu wa shule ya Kotinyang’ Mohamud Alnur anasema zaidi ya wanafunzi 800 hawatakuwa na sehemu ya kusomea baada ya paa zote za shule kungolewa na upepo mkali.
“Zaidi ya Wanafunzi 800 kutoka shule hii ya Korinyang’ itawalazimu kukaa nyumbani hadi pale serikali itajenga upya paa za shule hii kwani hawatakuwa na mazingira Bora ya kusomea” alisema Mwalimu mkuu Mohamud Alnur.
Mvua hiyo ambayo bado inaendelea kunyesha kwenye Kaunti ya Turkana haswa Turkana Kusini imekuwa ikiangusha miti mikubwa iliyokuwa ikitumika na wanafunzi kama kivuli, nyingine iking’olewa.
Paa za Madarasa ziling’olewa na hata kutikisa kuta za vyumba vingi huku kuta za darasa la nane pamoja na makao ya walimu kuharibiwa.
“Hakuna hata kiwanja ambayo watoto wanaweza kutembelea hapa. Ile kitu imefanyika watu ya forest mkuje mutusaidie” Eunice Ekori, Mwanakamati wa Shule alisema.
Mwakilishi wa wadi ya Katilu Etubon Samak anasema wakazi wa vijiji vya Lopur, Kambi Baraka, Namibia na Angarabat pia wamepata hasara kubwa mno,mvua ikiharibu nyaya za umeme, makazi na mifugo wao kufa baada ya kuzidiwa na mvua kubwa.
Etubon anasema baadhi ya vifaa muhimu katika Hosipitali ya Katilu viliharibiwa na mvua akitaka serikali kuhakikisha inanusuru hali katika Hosipitali ya Katilu.
“We don’t have electricity, all surgical operations cannot be conducted, laboratory tests in the hospital is unavailable due to power outage” alisema Mwakilishi Wadi ya Katilu Samak Etubon.
Wakazi wameitaka serikali kuhakikisha inajenga upya shule ya Korinyang’ na kurekebisha paa za Madarasa zilizoharibiwa na upepo mkali kabla ya wanafunzi kurejea shuleni kwa muhula wa pili juma lijalo.
Story by Kitio Micah