Watu kadhaa wamejeruhiwa kufuatia ajali ya barabarani katika Barabara ya Kisii-Kaplong, mapema Jumapili.

Kulingana na walioshuhudia basi hilo lililokuwa likielekea eneo la Nyamarambe kutoka Kisii, lilikuwa likijaribu kuepuka kugongana na lori lililokuwa likitoka upande mwingine wakati dereva alipoteza mwelekeo na kusababisha lianguke.

Inaarifiwa dereva wa basi alikuwa akijaribu kulipita gari jingine wakati wa ajali hiyo. Basi lililohusika katika ajali lilikuwa likiwasafirisha abiria katika maeneo mbalimbali ya Kisii.

Polisi wanasema uchunguzi unaendelea kwani unahofiwa kuwa huenda kuna abiria waliojeruhiwa vibaya.

Ajali hiyo ni ya hivi punde kutokea katika barabara ya Kisii-Kaplong ambayo imetajwa kuwa hatari kwani ajali nyingi huripotiwa.

Mapema mwezi Machi watu watano walifariki dunia kufuatia ajali kwenye barabara iyo hiyo.