Polisi katika eneo la Lokichogio wamefanikiwa kuwakamata wanaume wawili waliopatikana wakimiliki silaha kinyume cha sheria.
Wawili hao Lopua Ekuyen mwenye umri wa miaka kumi na minane na Lokal Chara mwenye umri wa miaka kumi na tisa walitiwa mbaroni baada ya wananchi kuwaarifu polisi. Vijana hao wlaipatikana na bunduki aina ya AK-47 na maganda ya risasi.
Wawili wanaendelea kuzuiliwa na polisi huku uchunguzi ukiendelea kabla ya kufikishwa mahakamani.
Bunduki na maganda hayo pia vinazuiliwa na vitatumika kama ushahidi.