Ndege ya Shirika la Kenya Airways KQ iliyokuwa ikielekea Dar es Salaam, Tanzania ililazimika kurudi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta JKIA, Jumapili kutokana na dharura ya kiafya.

Taarifa ya KQ ilisema ndege ya KQ484 illiyoondoka Nairobi hadi Jiji kuu la Tanzania, ilirudi JKIA muda mfupi baadaye kutokana na dharura hiyo.

Wakati ndege ilipowasili, ilipokelewa na wahudumu wa afya na taratibu muhimu za kiafya na usalama zilizingatiwa.

KQ ilisema, “The aircraft, which was operating from Nairobi to Dar es Salaam, returned to Jomo Kenyatta International Airport (JKIA) at approximately 13:40 local time, shortly after departure, due to a medical emergency.”

Taarifa hiyo aidha ilifafanua kuwa baadaye baada ya tatizo hilo kushughulikiwa ndege hiyo iliruhusiwa kurejea safarini kuelekea Tanzania mwendo wa saa saa tisa na dakika hamsini na nne mchana

Sehemu ya taarifa hiyo ilifafanua, “Passengers were briefed and provided with guidance in line with health and safety regulations. Upon attending o the emergency, the flight was cleared for taker to Dar es Salaam at 15:54hrs.”

KQ ilimalizia kwa kuwaomba radhi wateja wake ikisema usalama wao daima utafanywa kipaumbele.

“The safety and well-being of our guests and crew remain our highest priority. We sincerely apologise for the inconvenience caused and appreciate the patience and understanding of our guests during this period.”  Taarifa hiyo ilisema.