Profesa Makau Mutua amekubali uteuzi wa Rais William Ruto kuwa Mshauri wa Masuala ya Katiba katika Ofisi ya Rais, licha ya kauli zake za awali ambapo aliapa kutoshirikiana na Ruto.
Mutua, ambaye alikuwa msemaji wa kampeni ya Azimio la Umoja na mshirika wa karibu wa Raila Odinga, sasa amejiunga rasmi na serikali kupitia uteuzi huo.
Akikubali uteuzi huo, Mutua alisema, ”I am grateful to His Excellency President William Ruto for appointing me Senior Advisor on Constitutional Affairs in the Executive Office of the President.”
Aliongeza na kusema, atafanya kazi yake kwa njia ya uadilifu ”Our Constitution is the beating heart of the Republic. Mr President, I promise to serve you and our fellow citizens with diligence, honor, and distinction.”
Rais Ruto, katika taarifa ya Jumatano jioni, alimtaja Profesa Mutua kuwa mtaalamu mahiri katika masuala ya kisheria, kikatiba na haki za binadamu, akisema uteuzi wake unalenga kuimarisha utekelezaji wa Ajenda ya Mageuzi ya Kiuchumi ya Bottom-Up.
“Congratulations Prof Mutua. I welcome you to join a dynamic team of public servants in the implementation of our Bottom Up Economic Transformation Agenda,” Ilisema sehemu ya taarifa ya Rais Jumatano jioni.
Uamuzi wa Mutua kujiunga na serikali unajiria miezi michache baada ya Ruto na Raila kusaini mkataba wa ushirikiano, hatua iliyowapa viongozi kadhaa wa upinzani nafasi serikalini.
Miongoni mwa walioteuliwa ni Jaoko Oburu Odinga, mwanawe Seneta wa Siaya Oburu Odinga, katika nafasi ya Mshauri Maalum wa Masuala ya Uwezeshaji Kiuchumi.
Prof. Mutua, ambaye pia ni raia wa Marekani na Kenya, ni msomi wa masuala ya sheria na aliwahi kuwa Mkuu wa Chuo cha Sheria cha SUNY Buffalo, Marekani.