Aliyekuwa Waziri wa Usalama, Fred Matiangi ametangaza rasmi kuwania kiti cha Urais mwaka 2027.
Akiwahutubia wananchi mjini Keroka wakati wa ziara yake ya kwanza ya umma tangu aliporejea nchini kutoka Marekani, Matiang’i amesema amesikiliza sauti nyingi za Wakenya na ameitikia wito huo. Matiang’i amesema kwama yuko tayari kulikomboa taifa hili .
Maelfu ya wakazi walijitokeza leo kumkaribisha matiang’i katika ziara ya eneo zima la Gusii aliyoiita ”Meet-the-People.”
Matiang’i alisema hivi, “I want to tell you this, my friends, we have many challenges, but I want to ask you, please, let us not lose hope in our country. Our nation is built on resilience, so let us unite together so that we can move forward. Aliendelea kuuliza, ”will you allow me to talk to all Kenyans from all the counties?” huku wananchi wakishangilia.
Waziri huyo wa zamani amezunguka eneo zima la Gusii leo hii ikiwa ni Kaunti ya Nyamira na Kisii akipitia miji mbalimbali kama Kisii, Keumbu, Keroka, Kijauri na mingine.


Akiwa mjini Kisii umati wa watu uliojitokeza ulimlazimu kuhamishia hotuba yakekutoka kandokando ya barabara hadi Uwanja wa Gusii kwani kulikuwapo na msongamano wa watu ulioathiri shughuli.
Matiang’i aliandamana na viongozi wa eneo hilo la Gusii akiwamo Gavana wa Kisii Simba Arati mwenzake wa Nyamira, Amos Nyaribo, Seneta wa Kisii Richard Onyonka, Wabunge na wawakilishi Wadi.
Ziara hii inajiri siku chache tu baada ya Matiang’i kuungana rasmi na viongozi wa upizani; aliyekuwa Naibu wa Rais Rigathi Gachagua, Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka, Martha Karua, Eugene Wamalwa, Justin Muturi, Mithika Linturi na Mukhisa Kituyi.
Viongozi hao wanaojiita ”The People’s Opposition” walidai baada ya mkutano wao kuwa ndio watakaoleta mabadiliko katika uongozi nchini. Hata hivyo, Muungano huo umeshtumiwa na baadhi ya wadadisi na wasomi wakiuita usio wa mabadiliko yoyote.
Matiang’i akitangaza rasmi nia yake ya kujitosa kinyang’anyoroni 2027 inasubiriwa kuona iwapo wenzake wa upinzani watamuunga mkono ikizingatiwa baadhi yao akiwamo Kalonzo na Karua pia huenda wakajitosa uwanjani.
Swali kuu ni Je, Matiang’i atapata uungwaji mkono? Muda utabaini.