Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe amefafanua kwamba hakuna kampuni ya sukari iliyouzwa, akisisitiza kuwa uliofanywa ni ukodishaji tu. Kagwe amesema kwamba mchakato huo ulifanywa kwa njia ya uwazi na uliidhinishwa na bunge.

Akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge la Kitaifa ya Kilimo, Kagwe amefutilia mbali madai kwamba mpango huo wa ukodishaji haukufanyika kwa uwazi akisema washikadau wote walihusishwa kuanzia mwanzo.

Kagwe alisema hivi “No sugar factory has been sold. It’s leasing that has been done, and Parliament approved the whole process. I dismiss assertions that the process was opaque considering all stakeholders were involved. We are ready to submit any document for scrutiny by Parliament and the general public, as requested by Hon. Ruth Odinga, to assure the public on the lease process.

Akiunga mkono matamshi hayo ya Kagwe Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, John Mutunga amesema mpango huo ulifuata sheria na na kupigwa msasa na bunge.

“The sugar leasing process was taken through Parliament; that’s why other members are not worried. The leasing process was not restricted,” Alisema Mutunga.

Ufafanuzi huo unajiri wakati ambapo maswali mengi yameulizwa kuhusu hatima ya kampuni za sukari zilizokuwa zinamilikiwa na serikali na ambazo tayari zimekodishwa kwa wawekezaji wa binafsi..

Waziri Kagwe ametoa hakikisho kwamba serikali imejitolea kuwajibika na i tayari kutoa taarifa zote kuhusu jinsi mpango huo ulivyofanyika.