Rais William Ruto amefutilia mbali uteuzi wa wenyeviti wa kampuni za sukari za Chemelil, South Nyanza (Sony) na Nzoia.

Katika notisi kwenye Gazeti Rasmi la Serikali ya tarehe 12, Mei 2025, Rais alifutilia mbali uteuzi huo ili kuhalalisha mpango wa hivi majuzi wa ukodishaji wa kampuni za sukari zilizokuwa zinamilikiwa na serikali kwa wawekezaji wa binafsi.

Uteuzi wa John Nyambok, Jared Odhiambo Opiyo na Alfred Khang’ati’s kama wenyeviti wa kampuni za Chemelil, South Nyanza (Sony), na Nzoia Sugar umefutiliwa mbali mara moja.

Tayari serikali imekamilisha ukodishaji wa kampuni nne za sukari kwa lengo la kuimarisha sekta hiyo ambayo imedidimia kwa muda mrefu.

Ijumaa iliyopita Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe alitangaza kuwa wizara ilikuwa imefanikisha shughuli hiyo ya ukodishaji wa miaka thelathini wa kampuni hizo kwa wawekezaji wa binafsi.

Katika mpango huo mpya Kampuni ya Sukari ya West Kenya itachukua usimamizi wa ile ya Nzoia, Kibos Sugar and Allied Industries Ltd itasimamia kampuni ya Chemelil na Busia Sugar Industry nayo ikipewa usimamizi wa kampuni ya Sony Sugar Company, huku West Valley Sugar Company Ltd ikitakiwa kusimamia kampuni ya Muhoroni Sugar Company.

Wakati uo huo, waziri huyo wa kilimo alitangaza kufutilia mbali uteuzi wa wanabodi wa kampuni hiyo, akisema “I would like to assure the public and all stakeholders that the negotiated terms represent the best possible outcome to ensure the revival of the sugar sector,” CS Kagwe said. “I call upon your continued support in realising this vision. The Ministry remains fully committed and ready to address any concerns that may arise.”

Waziri Kagwe pia aliuhakikishia umma kwamba mali yote inayomilikiwa na kampuni hizo nne ikiwamo ardhi itasalia kuwa mali ya serikali.