Rigathi Gcahagua amezindua rasmi chama chake cha kisiasa cha Democracy for Citizens Party (DCP).
Kauli mbiu ya chama hicho ni ‘Sikiza Wakenya’, huku Gachagua akisema kuwa Wananchi wako huru kuibadilisha akisema hivi, ”Kenyans can always interchange it with ‘Sikiza Ground’. Gachagua amesisitiza ”Our party symbol is a ‘listening ear’, because we believe every Kenyan must be listened to by their leaders.”
Wakati uo huo, amesema hakutuwa na mapendeleo chamani kwani Chama cha DCP kitakuwa cha wakenya wote ”I want to assure all political aspirants in our party that we will not favour any candidate. We will get our candidates from the people of Kenya. The DCP Party will not give direct nominations to anyone; let the candidates meet each other on the ground.”
Sio hayo tu, Gachagua amesema vijana ndio watakaofanywa kipaumbele ndani ya chama hicho ”Today, among the top officials we are unveiling are Millennials and Gen Zs who will lead our Democracy for Citizens Party (DCP).”
Amewahakikishia Wakenya kwamba atawasikiliza wote bila kuzingatia misingi ya kikabila kauli inayoonekana kupuuza mtazamo kuwa yeye ni kiongozi wa eneo la Mlima Kenya. ”As the party leader of DCP, I commit to listening to Kenyans, irrespective of tribe, religion, or colour.”
Amesema katika kipindi cha miaka miwili ijayo atazunguka kote nchini kuwasikiliza Wananchi.
Katika uzinduzi huo, Gachagua amewataja viongozi wakuu wa chama huku akitangaza kuwa uzinduzi rasmi utafanyika Juni, 4 mwaka 2025 katika eneo atakalotangaza baadaye. Cleophas Malala aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha UDA sasa ndiye Naibu Kiongozi wa Chama cha Gachagua hicho cha DCP.
Viongozi wengine ni Mwenyekiti wa Mipango ya Kamati ya Kitaifa chamani Mithika Linturi ambaye pia alijiuzulu kutoka chama cha UDA. Cate Waruguru ndiye atakayekuwa Kiongozi wa Wanawake huku Maina Kamanda akiteuliwa Mwenyekiti wa watu wenye ushahwishi ndani ya chama cha DCP.
Katibu Mkuu wa muda wa Chama hicho atakuwa Hezron Obatah na Martha ole Kamwaro ndiye atakayekuwa Naibu Katibu wa DCP. Mweka Hazina wa kitaiifa ni Hannah Mutua, naibu wake akiwa Wanjira Njoka.
David Njenga Gikonyo ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa wakenya walioko Ughaibuni na Mshirikishi wa Kitaifa atakuwa Alex Amasi. Brendea Wanjira ameteuliwa kama Mkurugenzi Mkuu, na Christopher Mwadime Katibu wa Masuala ya Ugatuzi huku Mercy Gakuya akipewa nafasi ya Katibu wa Elimu.
Wengine ni Albina Kamwaga ambaye amepewa nafasi ya Katibu wa Masuala ya Kimataifa, Hessein Athumani katibu wa utalii na John Maraga atawawakilisha watu wenye ulemavu ndani ya chama cha Democracy for Citizens Party (DCP).