Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi EACC imepuuza madai kwamba kesi inazochunguza hasa zinazowahusu viongozi zinachochewa kisiasa. Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume hiyo Abdi Mahamud amesema tume hiyo inafuata sheria na inazingatia ushahidi unaowasilsihwa kwake na idara zinazohusika kabla ya kuanza kuwachunguza washukiwa.
”The commission (EACC) is not driven by any political agenda; what we do is follow the evidence,” alisema Mahamud.
Akionekana kulenga kesi ya hivi punde ya ufisadi dhidi ya Gavana wa Trans Nzoia, George Natembeya, Mahamud amesema inasikitisha kuona kuwa watu wanaolalamikia kuhusu wizi wa mali ya umma, ndio ao hao wanaolalamika wanapoanza kuwachunguza washukiwa. Amesema hivi ”The people who complain that public funds are being stolen, probably are the same people who feel that the commission is going overboard.”
Aidha amelalamikia jinsi baadhi ya Wakenya wanaochukua miegemeo kuhusu kesi za ufisadi akisema misimamo kama hiyo inaibua maswali mengi kuhusu maadili ya jamii -akisema ”What we are seeing is that, as long as it does not concern you or someone close to you, then it should be investigated; but when it concerns you or someone close to you, then corruption should not be investigated; anyone who tries to investigate then he/she is driven by politics or other forces, I think that is a wrong thing to do”
Amawataka viongozi hasa wanasiasa kuelewa namna tume hiyo inavyofanya kazi na kuisaidia kutekeleza majukumu yake badala ya kuishtumu kila wakati
Kauli ya EACC inajiri siku mbili tu baada ya kizaazaa kushuhudiwa nyumbani kwa Gavana Natembeya wakati wa msako wa maafisa wa tume hiyo na wale wa Idara ya Upelelezi DCI.

Makabiliano yalishuhudiwa baina ya maafisa hao na wananchi waliokuwa wakipinga kukamatwa kwa Gavana Natembeya, hali iliyosabbaisha uharibifu wa mali yakiwamo magari ya EACC na DCI. Tayari uchunguzi umeanzishwa kufuatia matukio hayo.
Gavana Natembeya alikamatwa Jumatatu na kufikishwa mahakamani Jumatano akikabiliwa na mashtaka ya ufisadi wa shilingi milioni 6. Gavana huyo alikana mashtaka dhidi yake na mahakama ikamwachilia kwa dhamana ya shilingi nusu milioni pesa taslimu au bondi ya shilingi milioni moja.
Aidha mahakama ilimzuia kuingia ofisini mwaka kwa kipindi cha siku sitini wala kuwasiliana na mashahidi.