Maafisa wa polisi mjini Kitale, Kaunti ya Trans nzoia,wanaendeleza uchunguzi kufuatia kifo cha mwanamme mmoja ambaye mwili wake umepatikana ukiwa na majeraha usoni kwenye Mto Sabwan katika kijiji cha Pombo, Eneo Bunge la Kwanza.

Kwa mjibu wa Fridah Marumbo ambaye ni mmoja wa wanakijiji, marehemu kwa jina Enock Omwoyi alikumbana na mauti baada ya kuwapeleka ng’ombe malishoni siku ya Jumatano kwenye shamba lililokuwa karibu na mto huo.

” Enock alikuwa katika shughuli zake za malisho ambapo Ng’ombe aliyekuwa nao waliingia kwenye shamba la mahindi na kuharibu kwa kiasi mimea ya mahindi iliyokuwa imepandwa mkabala na eneo la malisho,hatua ambayo inadaiwa kuwakasirisha baadhi ya watu waliokua karibu na eneo hilo, hatua ambayo inadaiwa kuzua mzozo ambayo ilipelekea marehema kufukuzwa kutoka eneo hilo hadi kwenye mto,hali ambayo anadai ilkua mara ya mwisho marehemu kuonekana akiwa hai”.

Ni hali ambayo imewagadhabisha pakubwa wanakijiji ambao wameitaka Idara ya Upelelzi DCI kuingilia kati na kufanya uchunguzi wa kina utakaobaini kilichosababisha kifo cha mwanamme huyo ambaye ni baba wa mtoto mmoja.

”Tungependa sana kujua kilichopelekea kifo cha Enock ambaye alikuwa mvulana mwenye tabia nzuri ambapo alifanya kazi yake kwa njia nzuri pasipo na kukosana na yoyo”alisema mmoja wa wanakijiji Crisantus Makori Nyamatura.

Akizungumza na Radio 47 kwa njia ya simu Kamanda Mkuu Polisi wa Kaunti Ndogo ya Kwanza Fred Abuga amesema tayari uchunguzi wa kina umeanzishwa ili kubaini chanzo cha kifo ya mwanamme huyo.

Written by, Isaac Famba