Polisi wangali wanachunguza kisa ambapo mwanamke aliteketea hadi kufa akiwa nyumbani kwake katika Eneo Bunge la Kimilili, Kaunti ya Bungoma.
Mwanamke huyo Christine Sifuna mwenye umri wa miaka 53 alifariki dunia usiku wa kuamkia Jumanne.
Kulingana na wakazi wa eneo hilo Wakiomgozwa na Dan Manyasi, kisa hicho cha usiku wa kuamkia Jumanne kilitokea mwendo wa saa nne na walishindwa kuthibiti makali ya moto uliokuwa ukisambaa kwa kasi.
Hata hivyo, wamekisia kuwa kisa hicho ni cha kupangwa wakitaka uchunguzi wa kina kufanywa ili kubaini kifo cha mama huyo wakitupilia mbali uwezekano wa hitlafu ya ngumu za Umeme.
“Moto ukiwaka majirani wakija bulbs za nyumba zilikiwa zinawaka,kwa hiyo hakuna uwezekano wa kuwa kifo hicho kilitokana na nguvu za umeme,jambo la pili tunaelezwa kuwa huenda moto ulisababishwa na mtungi wa gesi ila ulikuwa bure.,,Tunachokitaka sasa hivi ni haki ya Mama Christine.”Alisistiza Manyasi
Mmewe marehemu amesema kuwa tukio hilo lilitendeka akiwa katika duka lao huku wakazi wa eneo hilo wakitoa wito kwa maafisa wa polisi kuharakisha uchunguzi kubaini chanzo cha moto ambacho bado kimesalia kuwa kitendawili.
Baadhi ya wakazi wamesema kuwa huenda marehemu aliuawa na watu wasiojulikana na kisha nyumba yake kuteketezwa.
Kamanda wa polisi Kaunti nNdogo ya Kimilili Victor Nzaka amesema kuwa uchunguzi umeanzishwa akiwaomba wakazi kuwa watulivu.
Written by Sostine Wanji