Maafisa wa polisi katika eneo la Mungania, Meru wamewakamata washukiwa wawili wa wizi. Katika tukio la kwanza maafisa wa polisi wa akiba NPR wanasema walisikia milio ya risasi katika kituo cha Kibiashara cha Mungania, na walipofika hapo walifanikiwa kumkamata mshukiwa aliyekuwa na bunduki aina ya AK-47 na gari linaloaminika kuwa la wizi ambalo mshukiwa anaaminika alikuwa akilitumia.

Mshukiwa mwingine alikamatwa muda mchache baadaye akiwa na bidhaa zinazoaminika kuwa za wizi.

Washukiwa hao wawili wanaendelea kuzuiliwa wakisubiri kufikishwa mahakamani, huku vifaa vilivyopatikana pia vikitarajiwa kufanikisha uchunguzi unaoendelea.