Shule ya upili ya Jera iliyoko Kaunti ya Siaya imefungwa kwa muda usiojulikana kufuatia maandamano ya wanafunzi wakilalamikia ukosefu wa chakula.

Shule hiyo inakumbwa na upungufu mkubwa wa chakula hali ambayo imesababisha Wizara ya Elimu kuwaagiza wanafunzi kurejea nyumbani.

Wakizungumza shuleni humo, wakuu wa wizara hiyo ya elimu wamewataka wanafunzi kuwa na subra wakati mamalimishi yao yanaposhugulikwa.

Baadhi ya walimu na wanajamii wanataka Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Moses Okanda kuhamishwa kutokana na uongozi mbaya.

Wanafunzi wanamlaumu mwalimu mkuu huyo wakisema usimamizi wake mbaya ndio umesababisha hali hiyo. Wakizungumza na Radio 47 Digital baadhi ya wanafunzi wameuliza maswali kuhusu alikokuwa mwalimu huyo maandamano yalipokuwa yakifanyika, ”mimi nauliza Principle yuko wapi hivi vitu vinapoendelea, inamaanisha anajua kile anafanya,” alisema mwanafunzi mmoja.

Mwanafunzi mwingine alisema hajakula tangu Alhamisi jioni akisema ”Jana tulikuwa tu ugali na soup leo tumeamka tukapewa maji moto, saa hii ni saa sita hata hakuna kitu tumekula,” alisisitiza.

Wanafunzi hao wamesisitiza kuwa anataka mwalimu mkuu huyo kuhamishwa wakidai amekuwa akiwadanganya kwa muda mrefu, ”sisi kitu tunataka ni Principal aende kila siku anatudanganyam jaba kila siku tunataka tu aende,” aliongeza mwanafunzi mwingine.

Hata hivyo, watahiniwa wa mwaka huu wamesalia shuleni kuendelea na mtihani wa muigo uliokuwa ukiendelea.

Written by Michael Kwena