Titus Wekesa Sifuna amefikishwa katika Mahakama ya Milimani akiabiliwa na tuhuma za kumkosea heshima Rais William Ruto. Upande wa wa mashtaka umeomba azuiliwe kwa siku saba ili kuruhusu polisi kukamilisha uchunguzi unaoendelea.

Mahakama iliambiwa kuwa Sifuna ametumia akaunti yake ya X kwa jina @5thethief na jina”I must go”, kuchapisha matusi dhidi ya Rais na familia yake. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, machapisho hayo yamesababisha hisia kali miongoni mwa umma na yanachukuliwa kuwa tishio kwa amani na utangamano wa kitaifa.

Mahakama pia iliambiwa kuwa ujumbe na picha zilizochapishwa na mshukiwa zinachochea chuki na huenda zikachangia mgawanyiko wa kikabila.

Pia ilidaiwa kuwa Sifuna alibadilisha picha ya wasifu wa akaunti hiyo na kuweka picha ya Rais, jambo ambalo mamlaka zinasema linapotosha na ni hatari.

“Maudhui ya akaunti hiyo ya X ni tishio kubwa kwa heshima ya taifa, kwani Rais ni alama ya umoja wa kitaifa na anapaswa kuheshimiwa na kila Mkenya,” upande wa mashtaka uliiambia mahakama.

Upande wa mashtaka uliiambia mahakama kuwa, “The content of the X account poses a serious threat to the country’s reputation, as the President is a symbol of national unity and should be respected and honoured by all.”