Hali ya taharuki imetanda katika Kijiji cha Maungu, Eneo Bunge la Voi, Kaunti ya Taita Taveta, baada ya watu wasiojulikana kuwavamia kisha kuwaua ngamia kwa njia ya kikatili.
Familia ya Hassan Ibrahim, ni moja ya wakazi ambao wameathirika na uvamizi huo na sasa inakadiria hasara ya takribani shilingi zaidi ya milioni moja na laki nne.
Ibrahim, mwenye asili ya Kisomali ameelezea hofu ya matukio ya kutisha ya kuuliwa kwa hali ya kikatili ngamia nyakati za usiku, wa hivi punde akiwa ngamia wake wa saba chini ya miezi sita ambapo wiki hii ngamia wawili wameuliwa. Amesema hali hiyo inawatia wasiwasi wakihofia usalama wao.
Amesema “Tumeripoti Polisi visa hivi na sisi tunataka haki, sisi pia ni wakenya kama wakenya wengine. Tunalipa ada ya mbuga na tunatoa ushuru, Watoto wetu wanasoma hapa Maungu.”
Kulingana na familia hiyo, tukio hilo ni la kijambazi kwani ngamia hao wamevamiwa wakiwa katika Boma ndani ya ranchi ya Sagala ambapo hupelekwa malihsoni na kulala usiku kucha.
“Tumefanyiwa dhuluma kubwa na mifugo wetu hawakuingia kwa shamba ya mtu wako ndani ya mbuga. Ngamia huyu alikua ndani ya boma akafukuzwa na kukatwa mguu, ikakatwa shingo na ikaanguka.” Alisema Ibrahim.
Ahmed Mahad, Mfugaji wa ngamia ameitaka serikali na taasisi za usalama kuchukua hatua za dharura kuwakamata washukiwa na kuwachukulia hatua za kisheria.


Abdirahman Hassan ambaye ni mchungaji wa ngamia amesema wamehangaishwa na kwa wiki hii pekee ni ngamia wawili wameangamizwa kwa kuuliwa jambo ambalo amesema sasa linatishia usalama wao.
“Katika wiki hii ni ngamia mbili, kwa mwezi sasa ni ngamia tatu, chini ya mezi sit ani ngamia saba. Tunataka serikali itusaidie.” Alisema.
Kwa upande wake Idris Mohammed, Mwanaharakati na Kiongozi wa kijamii katika eneo la Maungu amekemea matukio hayo akitaka Wizara ya Usalama na Ile ya Kilimo na Ufugaji kuingilia suala hilo kwani imekua tishio kwa Usalama wa Wafugaji ambao wamekua wakifanya shughuli zao za ufigaji kwa zaidi ya miaka ishirini.
Alisema hivi, “Tungetaka asasi za usalama kuchukua hatua za haraka na kuwakamata washukiwa na kuchukuliwa hatua. Kwa sasa Ngamia saba wameuliwa na Ngamia mmoja ni shilingi laki mbili kwa jumla ni hasara ya zaidi ya shilingi milioni 1.4. Ni hasara kubwa ikizingatiwa jamii yetu hutegemea ufungaji kujikimu ki uchumi.”
Hata hivyo wamesema wamepiga ripoti katika Kituo cha Polisi cha Maungu wakitarajia uchuguzi kuaza mara moja.
Written by, Julius Mariki