Cleophas Malala amepata pigo baada ya mahakama kudumisha uamuzi wa kuondolewa katika nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama cha UDA.

Akitoa uamuzi huo Jaji Bahati Mwamuye ametupilia mbali aumuzi wa Jopo-kazi la Kutatua Mizozo ya Vyama vya Kisiasa uliomrejesha Malala katika wadhfa huo.

Mahakama imesisitiza kuwa notisi iliyochapishwa katika gazeti rasmi la serikali iliyomwondoa Malala ni halali na itaendelea kutekelezwa.

“The first respondent’s appeal before the PPDT is hereby terminated and shall not proceed before the tribunal. Any orders previously issued in favour of the respondent are hereby vacated,” umesema uamuzi huo.

Malala aidha amepata pigo jingine baada ya uamuzi uamuzi mwingine katika mahakama hiyo kutupilia mbali mchakato wowote uliofanywa awali wa jopo kazi hilo la vyama vya kisiasa hivyo kuifunga mianya yote ambayo Malala angetumia kupinga kuondolewa kwake.

Uamuzi huo sasa unamaanisa Hassan Omar ndiye Katibu Mkuu rasmi wa UDA.

Omar, aliyekuwa Seneta wa Mombasa ni mwandani wa karibu wa Rais William Ruto.