Katibu Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi COTU Francis Atwoli, ameidhinishwa na Bodi ya COTU kwa muhula wa sita wa uongozi. Uamuzi huu ulifikiwa kwa kauli moja na viongozi wa vyama tanzu vya wafanyakazi, waliompongeza kwa uongozi wake wa muda mrefu na mchango wake katika kutetea maslahi ya wafanyakazi nchini.
Viongozi hao akiwamo Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Viwanja vya Ndege wamesema Atwoli umeleta mafanikio makubwa, ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushawishi wa COTU katika masuala ya kitaifa na kimataifa, pamoja na kuboresha mazingira ya kazi.
Kauli hizi zinajiri siku chache tu baada ya Atwoli kutoa kauli iliyoashiria kuwa huenda akastaafu hivi karibuni.
Aidha viongozi hao wamefafanua kuwa kauli ya Atwoli Jumamosi kuwa atastaafu ilinukuliwa visivyo.
“We want to tell those who are pushing for him to retire that he is still energetic and visionary. He has what it takes to steer the labour movement forward.” alisema Ndiema
Atwoli aliyetetea uongozi wake katika COTU alisema kasoro katika sekta ya Leba nchini itaonekana atakapoondoka madarakani.