Familia moja mjini Machakos imeachwa na mshutuko baada ya punda wao kuwageuka na kumuuma mama na mwanawe
Selina Ndinda aliyeumwa anasema punda huyo ilimuuma na kumjeruhi mikono yote miwili siku ya ijumaa kabla ya kumgeukia mwanawe wa umri wa miaka thelathini na minane kwa kumuuma na kumvunja mguu ambaye kwa sasa amelazwa katika hospitali ya Machakos Level 5
Anasema alikwenda kuzuia punda wake kupigana na mwenzake wa jirani na katika harakati hizo aliteleza na kuanguka ndipo punda huyo alipomgaragaza chini na kumuuma
Kutokana na matukio hayo Selina ana uoga wa kukaa na punda huyo na sasa anataka wataalamu wa mifugo kumpa ushauri.
Anasema tangu azaliwe hajaona punda akimng’ata binadamu na kumjeruhi.
Ndinda hata hivyo anasema kupata dawa ya kichaa yaani Rabbies katika hospitali ya Machakos Level 5 imekuwa vigumu na anahitaji shilingi alfu tano kununua kiwango cha kutosha cha dawa hiyo kumtibu mwanawe.
Aidha naye anahofia afya yake akisema hajawahi kupew chanjo ya kichaa cha mbwa ‘’rabbies’’.
Wakaazi walioshuhudia visa hivyo wanasema sio nadra punda kumuuma mtu hasa akiwa na haja ya kimwili (on heat)
David Musembi mkaazi mwingine anasema punda asipofanyishwa kazi basi hugeuka kuwa mnyama hatari.
Akithibitisha kisa hicho chifu wa eneo la Kathekakai Daniel Maweu anasema sio jambo la kawaida mnyama wa nyumbani kumng’ata binadamu
Anasema maafisa wa kilimo katika Kaunti ya Machakos walifika katika eneo hilo na kuwataka wakazi kufahamu hatua ya dharura ya haraka wanappumwa na mnyama wa kufuga.
Written by, Nicholas Mbai