Maafisa wa upelelezi wawakamata wawili ziadi wa maujai ya Mbunge wa Kasipul, Charles Ong’ondo Were.
Katika taarifa Idara ya Polisi imesema wawili hao ni Edwin Odhiambo maarufu Abdul Rashid na Dennis Sewe Munyasi.
Baada ya kukamatwa kwa washukiwa hao waliwaelekeza polisi hadi kwa nyumba moja eneo la Chokaa, Mtaani Kayole baada ya msako wa siku nzima, ambapo bastola mbili zinazoaminika kutumika katika mauaji hayo pia zilipatikana.
Aidha polisi wanasema walipata begi na viatu alivyofaa mshukiwa mkuu siku ya mauaji hayo. Kulingana na polisi kupatikana kwa vitu hivyo ni hatua kubwa katika uchunguzi wa mauaji ya Mbunge Ong’ondo Were.
“This is a breakthrough because the recoveries are key in the case.”

Uchunguzi wa awali wa risasi zilizopatikana katika mwili wa mbunge huyo, ulionesha kuwa silaha zilizotumika zilikuwa pia zimetumika katika visa vya uhalifu katika maeneo ya Komarock na Kayole jijini Nairobi, pamoja na Ndumberi, Kaunti ya Kiambu.
Were aliyekuwa akihudumu katika muhula wake wa pili aliuliwa kwa kupigwa risasi Aprili, 30 katika kile kinachoaminika kuwa ni tukio lililokuwa limepangwa.
Tayari washukiwa wanne wanaohusishwa na mauaji hayo wamekamatwa na wanaendelea kuzuiliwa uchunguzi ukiendelea.
Mshukiwa mmoja alipatikana na shilingi 615,000 nyumbani kwake jijini Nairobi, pesa zinazoaminika zilitokana na malipo baada ya kutekeleza mauaji hayo.
Aidha polisi walifanikiwa kupata sare kadhaa za maafisa wa polisi na simu za rununu ambazo zinaendelea kuchunguzwa.
Washukiwa walio kizuizini ni pamoja na, William Imoli Shighali kw ajina lingine Omar Shakur, Juma Ali Haikal, Douglas Muchiri Wambugu na David Mihigo Kagame, ambao watasalia korokoroni kwa siku thelathini uchunguzi ukiendelea.
Stakabadhi za mahakama zinaonesha kuwa washukiwa walikuwa wakiwasiliana kabla ya maujai hayo. Camera za CCTV zilionesha kuwa mmoja wa washukiwa waliokamatwa alikuwa akimfuatilia Mbunge huyo kutoka Barabara ya wabera jijini Nairobi.
Kwa sasa polisi wanaendelea kuwatafuta washukiwa wengine akiwamo afisa wa polisi anayehusihwa na mauaji hayo.
Afisa huyo anaaminika alinunua laini mpya ya siku kupanga mauaji hayo na sasa laini hiyo haifanyi kazi.
Hayo yakijiri ibada ya wafu kwa ajili ya Mbunge huyo inafanyika leo katika Kanisa la Consolata Shrine, lililoko Westalnds, jijini Nairobi.
Ong’ondo Were atazikwa Ijumaa.